MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA LIWALE NDUGU TINA SEKAMBO AMETOA TUZO KWA WALIMU NA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI WA MSINGI NA SEKONDARI KWA MWAKA 2022
Leo tarehe 25. 02. 2023 zoezi la ugawaji tuzo kwa walimu na wanafunzi wa sekondari na msingi limefanyika, mgeni rasmi katika zoezi la utoaji wa tuzo hizo ni Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mh. Goodluck Mlinga.
Tuzo hizo zimegawiwa katika ukumbi wa sekondari ya kutwa Liwale.Mh. Mkuu wa Wilaya amempongeza Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Liwale kwa kutambua na kuwaekea mazingira mazuri walimu na kufanya kupata matokeo mazuri kwa mfululizo.
Amehamasisha serikali za vijiji kusapoti mchango wa vyakula katika shule ambazo zipo katika vijiji husika.Pia ametaka bodi za shule kutambua ma kutimiza wajibu wao.
Amewataka walimu kusimamia nidhamu kwa wanafunzi na kuhakikisha kudhibiti vitendo hatarishi kwa wanafunzi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2018 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.