Mkuu wa wilaya ya Liwale mhe. Goodluck mlinga amekagua utekelezaji wa kutengwa kupimwa na kumilikisha wafugaji maeneo rasmi kwaajili ya zoezi la ufugaji katika kata kimambi.
Mhe mlinga amesema kila mfugaji aliechangia zoezi hilo atapewa haki ya kumiliki kitalu kwa muda wa miaka kumi kwa sharti la kupanda nyasi na kuchimba kisisma ili kuzuia uzuzruraji wa mifugo na uharibifu wa mazao ya wakulima na hifadhi. Mhe. Mlinga ametoa rai kwa wafugaji kuendelea kuchangia ili zoezi la kuwapimia liendelee ili wamilikishwe maeneo hayo.
Mpaka sasa timu ya wataalamuimefanikiwa kupima vitalu 33 ambavyo vimegharimu shilingi 80, 362,000. Sawa na shilingi 2,435,212 kwa kila kitalu.
Mhe. Mlinga amempongeza mkurugenzi mtendaji ndugu Tina sekambo na timu nzima ya idara ya ardhi kwa kutekeleza zoezi hilo kwa muda mfupi na kwa uzalendo. Mhe. Goodluck mlinga amesisitiza kua wilaya ya Liwale imejipanga kuboresha mazingira ya wafugaji.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.