Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga leo ametembelea kijiji cha Makata Kitongoji cha Chekanenda na kutoa pole kwa familia pamoja na jamii baada ya mkazi wa kijiji hicho bwana Mohamed Shomari Kapuja umri wa miaka 45 kuuwawa na tembo.
Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa tatatizo ni kubwa na bado Serikali inazidi kupambana na tatizo hilo hili kuondoa changamoto iyo aidha pia amewakumbusha ahadi ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya kuchukua changamoto iyo na kwenda kuifanyia kazi katika ngazi ya kitaifa ili kuondoa changamoto iyo ya wanyama waharibufu tembo ambao wamekuwa wakileta madhara kwa jamii.
Aidha Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mlinga amesema jitihada zinazo chukuliwa na Wilaya ni kubwa kuhakikisha wanapambana na wanyama hao pia amewapongeza Taasisi ya wanyama pori TAWA kwajinsi wanavyo pambana na tembo kuhakikisha wanawatoa mbali na makazi ya watu lakini bado tatizo nikubwa ndani ya wilaya hii.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kuna mradi wa ambao umeisha tambulishwa na utatambulishwa hivi karibuni katika vijiji vyote ambao ni kati ya Serikali ya Tanzania pamoja na Serikali ya Ujerumani kwajili ya kupambana na tembo pamoja na wanyama haribifu na lengo la mradi huo ni kutoa mafunzo kwa wananchi pamoja na makundi na kutoa pia vitendeakazi kwajili ya kupambana na tembo.
Pia Mkuu wa Wilaya amewahakikishia wananchi wa kijiji cha Makata kuwa ataendelea kuwatumia askari wa wanyama pori pamoja na kusimamia miradi ambayo italetwa ili kuhakikisha wanakabiliana na tembo ambao ni waharibifu katika mazingira yetu na hata hivyo kwa tembo ambao wamekuwa wakiwauwa watu Mheshimiwa Mlinga amesema kuwa ataendelea kutafuta kibali ili kuwaondoa wasiendelee kuleta madhara kwa watu.
Nae mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Mohamed Mutesa ametoa pole kwa wananchi wa kijiji cha makata na kuwataka kuwa wastahimilivu kipindi hiki kigumu huku jitihada zikiendelea kuchukuliwa na serikali yao pia amwewataka wananchi kuhakikisha wanaacha kihifadhi mabibo ndani kwa msimu huu wa korosho tembo wamekuwa ni wengi wakifuta mabibo hivyo wanavyo sikia harufu ya mabibo basi wanakuja na pia amewataka kuchukua tahadhari pindi wanapokuwa wapo kwenye mashamba yao kwa msimu huu wa korosho.
Nae msimamizi wa Taasisi ya Wanyama pori TAWA Wilaya ya Liwale ndugu Chacha amewakumbusha wananchi wa vijiji vyote kuhakikisha wanachukua taadhari katika kipindi hichi na pia kutoa taarifa kwani kwa sasa kumekuwa na makundi ya tembo yanazunguka sehemu mbalimbali hivyo pindi wanapo yaona watoe taarifa kwa wakati kabla madhara ayajotokea.
Ndugu Chacha kutoka Taasisi ya wanyama pori TAWA akiwaelezea wananchi wa Kijiji cha Makata jinsi ya kuchukua taadhiri pindi tembo wanapokuwa wamevamia maeneo yao.
Mkuu wa wilaya ya Liwale Mhesimiwa Goodluck Mlinga pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri wakiwasikiliza Wananchi wa Kijiji cha Makata baada ya kifo cha mtu mmoja kilichosababishwa na tembo.
Wananchi wa kijiji cha Makata wakiwasikiliza wataalamu wa wanyama pori .
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.