Chama Kikuu cha Ushirika cha RUNALI kimeuza jumla ya kilo 21,825,459 za korosho katika mnada namba tatu wa msimu wa 2025/2026, uliofanyika leo katika Kituo cha Malipo cha RUNALI kilichopo Wilaya ya Liwale.
Katika mnada huo, bei ya juu iliyopatikana ilikuwa shilingi 2,700 kwa kilo, huku bei ya chini ikiwa shilingi 2,550 kwa kilo, hatua inayoonyesha kuimarika kwa ushindani miongoni mwa wanunuzi wa zao hilo.
Akizungumza mara baada ya mnada huo, Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mheshimiwa Goodluck Mlinga, amepongeza matumizi ya mfumo wa kidijitali unaotumika kuendesha minada ya korosho, akisema umeongeza ufanisi na kupunguza changamoto kwa wakulima.
Mheshimiwa Mlinga amewataka wadau wote, hususan vyama vya ushirika na taasisi za kifedha, kuhakikisha wanawalipa wakulima ndani ya siku saba kuanzia leo, ili kuwawezesha kupanga shughuli zao za kiuchumi bila ucheleweshaji.
Amesema kuwa Serikali haitavumilia tabia ya baadhi ya wahusika kuchelewesha malipo, kwani kufanya hivyo kunarudisha nyuma jitihada za kukuza uchumi wa wakulima wa korosho.
Katika hatua nyingine, Mlinga amewataka wakulima ambao hawatakuwa wamelipwa ndani ya muda uliowekwa kufika ofisini kwake au ofisi za uongozi wa ushirika ili kutoa taarifa. Amebainisha kuwa Serikali itachukua hatua kali dhidi ya watu watakaohusika na ucheleweshaji wa makusudi.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.