Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodcluk Mlinga amewataka wafanyabiashara na wananchi kufanya usafi katika maeneo yao ya biashara na kila ifikapo jumamosi ya mwisho wa mwezi kufanya usafi kwa Pamoja katika maeneo yote ya Mji.
Akizungumza na wafanyabiashara na vikundi vya mazoezi ya kukimbia(joging) katika viwanja vya Soko la Zeini katika kuazimisha siku ya usafi Duniani ambapo kwa hapa kwetu Tanzania imeanza kuazimishwa mwaka 2022, ambapo kwa mwaka huu yamelenga kuhamasisha taasisi mbalimbali kuungana na Jamii kushiriki maazimisho haya kwa kufanya usafi katika Mazingira yetu ya Liwale
Aidha Mheshimiwa asema kuwa kila mtu anapaswa kuhakikisha eneo lake linakuwa safi mara zote huku akitakiwa kuwa na kiwekea taka ili kuepusha uchafu kusambaa lakini pia siku ya jumamosi kwa umoja wetu tunatakiwa kuungana kufanya usafi na maduka yote yanapaswa kufunguliwa saa nne asubuhi baada ya kufanya usafi ili kuweka mazingira yetu kuwa safi.
‘’Ndugu zangu kama nilivyotambulisha mwanzo leo ni siku ya usafi Duniani na Tanzania tumeanza kuazimisha mwaka 2022 siku hii hukutanisha taasisi zote za kiserikali na binafsi pamoja na wananchi lengo la maazimisho haya nchini yamepangwa kufanyika katika Halmashauri ili kutekeleza shughuli zifuatazo kwanza viongozi na wananchi kushiriki shughuli za usafi katika Mazingira’’
‘’ Sambamba na hayo ni kutoa Elimu ya udhibiti wa taka kupitia mikutano ya hadhara na kutathimini kiwango cha taka zilizopo na kuchukua hatua hili ndilo nisema mwanzo hali ya usafi ni mbaya sana lakini pia kila jumamosi ya mwisho tufanye usafi kwani maadhimisho haya yanataka taasisi mbalimbali, viongozi na jamii kwa ujumla kushiriki usafi kama ilivyo ainishwa hapo juu ivyo jumamosi ya mwisho ya mwezi tutajipanga kwa makundi na tutakuwa na orodha ili kila kundi lifanye usafi’’.
Baadhi ya wananchi na Mkuu wa wilaya Mhe. Goodluck Mlinga walio jitokeza kufanya usafi siku ya usafi duniani wilaya ya Liwale
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.