MAFUNZO YA STADI ZA MSINGI ZA SHUGHULI ZA KIUCHUMI KWA WALENGWA WA TASAF.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha walengwa kuweza kujitegemea kiuchumi,Kuandaa mpango rahisi wa uanzishaji wa biashara na kuwapatia ruzuku ya uzalishaji kulingana na mpango wa biashara walioandaa Walengwa.
Ambapo walengwa baada ya kupata mafunzo kila kaya itanufaika na ruzuku kutoka TASAF ambayo watatumia katika mpango wa biashara walioandaa. Na ruzuku hizo hazitarudishwa.
Mafunzo hayo yamegusa maeneo mbalimbali ikiwemo namna ya kuandaa mpango wa biashara,Jinsi ya kupata masoko,Jinsi ya kupata wazo la biashara na Jinsi ya kutoa huduma.
Mafunzo hayo yamesimamiwa na muwezeshaji, Afisa Maendeleo ya jamii Maria Millanzi, yaliofanyika katika ofisi za kijiji cha Huria Kata ya Likongowele.
Walengwa wamepongeza serikali kupitia mradi wa TASAF, kwa mikakati mbalimbali ya kuboresha hali ya uchumi kwa walengwa wa TASAF.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2018 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.