KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANZANIA. MGENI RASMI WA KONGAMANO HILO MKUU WA WILAYA YA LIWALE MH. JUDITH NGULI.
Kongamano limehusisha mdahalo wa wanachi kuhusu hoja mbalimbali ikiwemo mafanikio yaliopatikana wilaya ya liwale.
Mgeni rasmi mh. Judith Nguli alifungua mdahalo huo kwa kuwapa nafasi wazee maarufu wa wilaya ya liwale kuelezea historia fupi kuhusu wilaya ya liwale, kuelezea mafanikio mbalimbali yaliopatikana ndani ya miaka 61 ya uhuru.
Aidha viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wamepongeza juhudi zilizofanyika na serikali kwenye kutekeleza miradi mbalimbali ya afya, elimu, umeme, maji na barabara. Pia wanafunzi walipongeza serikali kuweka miradi mbalimbali kwenye elimu hususani ujenzi wa madarasa. Pia wananchi waoichangia hoja zao kwenye maendeleo mbalimbali kwenye huduma za jamii, elimu na afya.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya liwale Mh. Mohammed Mtesa amewasisitiza vijana kuacha kukaa vijiweni na kutumia uhuru na fursa walizonazo kujikita katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kufanya kazi kwa bidii
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2018 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.