Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amesema kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya imependekeza mwekezaji ndugu Kassim Msosa apewe hekari 500 badala ya 1000 ambazo alizokuwa ameomba hata hivyo kamati imesama ndugu Msosa atakapo timiza ahadi ambazo amehadi kwenye kijiji cha Kichonda basi atapewa hizo hekari zilizo baki ili aendelee kuwekeza.
Aidha Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mlinga amewambia wananchi wa kijiji cha kichonda kuwa Serikali inatamani na inawapenda wawekezaji lakini kikubwa ni kuhakikisha wanatatua changamoto za wanakijiji wa Kichonda ikiwemo hizi ambazo amehahidi ndugu Kassim Msosa ili wananchi mpate huduma lakini tumejiridhisha kuwa msosa apewe kwanza hizi hekari 500-kwanza atuthibitishie uwezo wake kwa kutekeleza yale ambayo ametuhaidi.
Hata hivyo wananchi wakijiji cha kichonda wamemuomba mkuu wa wilaya Mheshimiwa Goodluck Mlinga kuhakikisha anawashauri vizuri na kusimamia ili waweze kumpata mwekezaji ambaye ata tatua changamoto zao katika kijiji cha Kichonda ikiwemo upatikanaji wa maji kwenye kijiji cha Kichonda.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.