Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mheshimiwa Goodluck Mlinga, amewapongeza madereva wa pikipiki (bodaboda) katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale kwa kudumisha amani wakati wote wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Urais, Wabunge na Madiwani uliomalizika hivi karibuni.
Mheshimiwa Mlinga ametoa pongezi hizo leo katika mkutano na madereva hao uliofanyika eneo la Mti Mkubwa, Kata ya Nangando, akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya (KUU). Katika hotuba yake, aliwahimiza madereva hao kuendelea kuilinda amani na kujikita zaidi katika shughuli za uzalishaji mali, ikiwemo uendeshaji wa pikipiki na kilimo, ili kujipatia kipato halali na kuboresha maisha yao.
Aidha, Mhe. Mlinga aliwataka madereva wa bodaboda kuwa waangalifu na kuepuka kutumiwa na wanasiasa wenye maslahi binafsi, akisisitiza kuwa serikali inaendelea kuwapa kipaumbele kupitia fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri inayotolewa kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.