• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Liwale District Council
Liwale District Council

Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Uhasibu
      • Miundo Mbinu
      • Afya
      • Usafishaji na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maliasili
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ufugaji wa Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Mifugo
    • Vivutio vya kitalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Ugani
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Mipango na Fedha
      • Uchumi na Mazingira
      • Community Services
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Mheshimiwa Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu
    • Miongozo mbalimbali
  • KItuo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi na kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

Baraza la Madiwani Limekutana na Kujadili Taarifa za Maendeleo

Imewekwa:: October 30th, 2023

Baraza la Madiwani limekutana katika Mkutano wa kawaida wa Baraza la Halmashauri ambapo ajenda kuu ni kuwasilisha taarifa za Kata, mapato na matumizi ya Kata na changamoto pamoja na kujadili miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale na kumpitisha mwekezaji katika Kata ya Kichonda   ambapo kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya, Kamati ya Ulinzi na usalama pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo.

Baraza la Waheshimiwa madiwani wamejadili juu ya changamoto ambazo zipo kwenye Kata zao ikiwemo changamoto ya nyumba za watumishi, wanyama waharibifu ambao wamekuwa wakiharibu mazao yao tembo, uvamizi wa mifugo katika maeneo ya wakulima, changamoto ya upatikanaji wa mawasiliano ya simu na mabweni ya wanafunzi.

Aidha wamepongeza jitihada zinazofanywa na watendaji wa Halmashauri katika kusimamia miradi ya maendeleo  na ukusanyaji wa mapato na kuomba kuongeza nguvu katika kukusanya ili mapato yatumike katika kuleta maendeleo pia wameongeza wakiomba kufanyiwa kazi changamoto zote ambazo zipo ikiwemo kuhakikisha hoja za wakaguzi zinajibiwa na kufutwa pia wameomba Halmashauri kuwasaidia katika miradi ambayo imekwama ili iweze kukamilika na kutoa huduma kwa wananchi, aidha waheshimiwa madiwani kwa pamoja wamekubali kumpitisha mwekezaji kupewa hekari 1000 katika eneo la Kata ya Kichonda.

Katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Goodluck Mlinga amewaeleza Waheshimiwa Madiwani na baraza juu ya miradi ambayo inatekelezwa na Serikali katika Wilaya ya Liwale ikiwemo kwenye ujenzi wa barabara, madarasa, usambazaji wa umeme vijijini, usimamizi wa maliasili za misitu, na madini pamoja na kusumami upande wa kilimo.

Pia Mheshimiwa Mlinga amewambia Waheshimiwa Madiwani jitihada zinazofanywa na Serikali katika kupambana na changamoto za uvamizi wa mifugo ambapo Wilaya ya Liwale imetenga eneo la  Kata Kimambi na kugawanywa kwa wafugaji na kuyaendeleza maeneo hayo kwa kupanda nyasi na kuchimba visima vya maji katika maeneo yao pia kwenye upande wa wanyama waharibifu tembo Mheshimiwa Mlinga amewaeleza Waheshimiwa Madiwani kuwa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani wameleta mradi wa GIZ ili kutuoa mafunzo na vifaa ili kupambana na wanyama hao waharibifu.

Aidha Mheshimiwa Mlinga amewataka Madiwani kuwa wasimamizi katika Kata zao na kuhakikisha kuwa wanawasimamia watumishi wote katika Kata zao na pia wakae kwenye vituo vyao vya kazi kwani wengi wao wamekuwa hawakai kwenye vituo vyao pia amewataka Madiwani kuhakikisha wanasimamia rasilimali za misitu kwenye maeneo yao kwani kumekuwa na uvunaju haramu na kutofuta taratibu na sheria katika uvunaji pia amewakumbusha kusimamia miradi ya maendeleo kwenye Kata zao.

Aidha Mkuu wa Wilaya amegiza Watendaji wa vijiji na Kata kuhakikisha wanasimamia shughuli za maendeleo katika maeneo yao na pia kusimamia ulinzi na usalama wa Kata na Vijiji kwani kwa sasa ni msimu wa korosho na hivyo matukio yamekuwa mengi sana watu wanaiba korosho kwenye mashamba hivyo amewataka wakawe walinzi kwenye maeno yao.

Picha mbalimbali katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Liwale.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO AWAMU YA PILI KWA MWAKA WA FEDHA 2024/2025 February 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MKATABA MSF May 07, 2025
  • TANGAZO LA KUANZA KWA MFUMO MPYA WA TAUSI KWA AJILI YA UTOAJI HUDUMA YA MALIPO MBALIMBALI YA SERIKALI KWA NJIA YA MTANDAO February 20, 2023
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI October 09, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI (BVR KIT) JIMBO LA LIWALE WAPATIWA MAFUNZO

    May 14, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA LIWALE YAPOKEA TUZO YA GLASS YA ELIMU KIMKOA KWA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA KWA MWAKA 2024

    May 02, 2025
  • UFUNGWAJI YA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA.

    November 01, 2024
  • MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA HALMASHAURI

    October 30, 2024
  • Angalia Zote

Video

Video nyingine

Viunganishi vya Haraka

  • www.tamisemi.go.tz
  • Kupata Hati ya Mshahara (Salary Slip) kwa Watumishi wa Umma
  • Bodi ya Ajira
  • Utabiri wa Hali ya Hewa
  • Taarifa za huduma ya elimu
  • Taarifa za huduma ya afya

Tovuti Linganifu

  • Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Linndi RS
  • Ruangwa
  • Nachingwea
  • Lindi Manispaa

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Dissertation-Writingservice.com

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters

    Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE

    Simu ya Mezani: 023 2937043

    Mawasiliano ya mkononi:

    Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz

Anuani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.