Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mheshimiwa Gooduck Mlinga amekutana na wafanyabiashra na wadau mbalimbali katika kujadili fursa za uwekezaji na changamoto zake katika Baraza la Biashara Wilaya ya Liwale.
Katika Baraza hilo wajumbe mbalimbali wameweza kuhudhuria ikiwemo Sekta binafsi, Taasisi za kifedha, Wajasiriamali wa aina mbalimbali pamoja na Taasisi za Serikali ambazo zipo ndani ya Wilaya ya Liwale ambapo wamejadili fursa zinazo patikana hapa na zinazotoka na kilimo, uchimbaji wa madini, mazao ya misitu pamoja na fursa nyingine.
Aidha wadau wa kilimo wameitaka Serikali kuhakikisha inatilia mkazo katika kuongeza mnyororo wa thamani katika zao la korosho ambalo ndio zao kubwa linalolimwa ndani ya Wilaya ya Liwale hivyo kuanzisha viwanda vya ubanguaji ili kuongeza thamani ya zao la korosho kwani huitaji ni mkubwa hivyo kutokana na kutokuwa na viwanda hatuwezi kuzalisha korosho nyingi ambazo zimebanguliwa na soko ni kubwa tunaiyomba Serikali pamoja na wadau wengine watusaidie ili tuweze kuwa wazalishaji wakubwa wa korosho.
Hata hivyo katika uzalishaji wa mazao mengine Wilaya ya Liwale imejikita katika kuhakikisha inawahamasisha wakulima kulima zao la alizeti ambalo linatumia mda mfupi na pia litasaidia kuongeza kipato kwa wakulima ukilinganisha kusubiri zao moja la korosho ambalo linalimwa msimu mmoja hivyo wadau hao wameitaka Serikali kuhakikisha inatumia jitihada katika kuhakikisha wakulima wanalima kutokana na soko lake kuwa la uhakika na pia kuwawavutia wawekezaji wakubwa ambao wanamitaji kuja kuanzisha viwanda vya ukamuaji wa mafuta ya alizeti.
Pia kupitia sekta ya ufugaji Wilaya ya Liwale imetenga maeneo kwa ajili ya wafugaji maeneo ambayao ni Kata ya Kimambi, Ndapata na Lilombe na kuwataka wawekezaji katika sekta hiyo kuanzisha na kuchimba visima kwa aajili ya wafugaji kipindi cha kiangazi wafugaji wengi huwa wanahama kwenda kutafuta malisho hivyo visima vitakuwa ni biashara wafugaji watanunua maji na kunywesha mifugo yao na pia kuanzisha majosho ya kuogeshea mifugo yao hivyo wadau wachangamkie fursa hizi.
Aidha wafugaji wameomba kupatiwa elimu ya ufugaji wenye tija ili kuhakikisha wanakuwa na mifugo ambayo wateweza kuimudu na kuhiudumia vizuri na pia wameomba Taasisi za kifedha ikiwemo mabenki yaweze kuwatambua na kuwakopesha fedha ili weweze kuwekeza na kufuga kibiashara zaidi na pia kuongeza uzalishaji hasa wa nyama na maziwa.
Kwa Wilaya ya Liwale pia fursa za mazao ya misitu zinapatikana kwa wingi hususa mbao za miti ya asili ikiwemo mikongo na mininga ambayo inapatikana hapa pia kuna miti mingine ikiwemo mitondoro na mipangapanga ambayo inazalisha samani za nyumbani na maofisini hivyo pia bishara ya mbao inafanyika tuwaombe wadau kuhakikisha watumia fursa hizi katika kukuza uchumi wa Liwale na kuleta maendeleo.
Aidha pia kwa Wilaya ya Liwale kuna fursa za uchimbaji wa madini aina ya dhahabu, jimstone, cristabell pamoja madini ya ulanga, na marble ambazo wadau wamejadili pamoja na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ili kuhakikisha kuwa sekta hiyo inatumika vizuri ili iweze kuleta matokeo chanya katika jamii na kuongeza uchumi wa Liwale.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mlinga amesema katika Baraza hilo hatahakikisha kuwa fursa zote zilizopo ndani ya Wilaya ya Liwale zinatangazwa kikamilifu ili wafanyabiashara waje na wawekezaji wakubwa pia ili kuongeza na kukuza uchumi wa Liwale kupitia fursa mbalimbali za uwekezaji katika Wilaya hii hata hivyo amezitaka Taasisi za Serikali kuhakikisha zinafanyia kazi na kutatua changamoto zote ambazo wadau wamezieleza hapa ikiwemo upande wa Halmashauri kusaidia upatikanaji wa mikopo kwa makundi maalumu ili waweze kuanzisha viwanda vidogovidogo vya kuongeza thamani ya mazao ikiwemo kubangua korosho na korosho soko lake ni kubwa hivyo tuchangamkie fursa hizi mapema.
Pia ameitaka Halmashauri kupitia Idara ya Biashara na Viwanda kuhakikisha inawasaidia wafanyabiashara na wawekezaji kuwa wanapewa elimu na kupata taarifa sahihi ili wajue kuwa fursa zipo na pia ameitaka Idara ya Maendeleo ya Jamii kuhakikisha kuwa inasaidia wajasirila mali wadogo hususa wanawake na vijana wanapata mitaji kwa kupitia mikopo inayo tolewa.
Aidha Mheshimiwa Mlinga amezitaka Taasisi nyingine kuhakikisha kuwa zinatatua changamoto za wawekezaji na wafanybiashara ambazo zimetajwa hapa ikiwemo upande wa Wakala wa Misitu tanzania TFS, TRA, Halmashauri pamoja na wadau wengine ikiwemo mabenki kutatua changamot hizo ili kusiwepo na ukwamishaji katika kufikia fursa hizo.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.