Thursday 5th, December 2024
@KATA YA NANJINJI KATA YA LIKONGOWELE
Picha mbalimbali za mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Nanjinji Kata ya Likongowele . Ambapo Mhe Waziri Selemani Jafo alikutana na wananchi kuwaeleza tathmini ya miradi ya maendeleo wilaya ya Liwale na kuwapongeza kwa kupokea miradi mingi ya afya na elimu.
Mhe. Dkt Selemani Jafo (mb) amefurahishwa sana kuona idadi ya vituo vya afya zimeongezeka kufikia 05, hospitali kubwa ya wilaya na zahanati 36. Pia miradi hiyo imekamilika ndani ya muda mfupi, amempongeza mkuu wa wilaya ya Liwale Mhe. Goodluck Mlinga kwa kusimamia vizuri miradi hyo.
Aidha mhe Waziri amewaasa wananchi kuishi kwa upendo na amani na kuacha vitendo vya unyanyasaji wa wanawake na Watoto.
Aidha mkuu wa wilaya ya liwale Mhe. Goodluck mlinga amemshukuru Mhe Waziri kwa kufanya ziara wilaya ya liwale na pia anajivunia kusimamia miradi hiyo na kumuahidi Mhe. Rais kuendelea kusimamia miradi hiyo kwa ufanisi kwa maslahi ya wananchi wa Liwale na Taifa kwa ujumla. Vivyo hivyo mbunge wa wilaya ya Liwale Mhe Zuberi Kuchauka amemshukuru mhe Rais kwa kutekeleza ipasavyo ilani ya chama cha mapinduzi mpaka sasa vijiji vyote vimewaka umeme, miradi ya elimu na afya imefikika kwa asilimia kubwa.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. BOX 23 LIWALE
Simu ya Mezani: 023 2937043
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2023 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.