Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe. Sarah Chiwamba aipongoza bodi, walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Liwale kwa ushirikiano na utendaji uliopelekea ufaulu wa juu katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2019.Aidha, katika kuwapongeza aliwaita walimu wote wa shule ya sekondari Liwale na kuitunuku shule cheti cha pongezi ikiwa ni ishara ya kuheshimu mchango wao katika maendeleo ya Elimu.
Mhe. Sarah Chiwamba alifanya haya wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Liwale tarehe 17 Julai, 2019 ambacho kilihudhuriwa na Mhe. (Mb) Zuberi Kuchauka, Waheshimiwa Madiwani, Wenyeviti wa vyama vya siasa, Wakuu wa Idara na Vitengo, viongozi wa dini na asasi za kiraia.
Awali, Mhe Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa kikao alipokea taarifa ya utendaji kazi wa Halmashauri na Taasisi za Umma kwa kipindi cha mwaka Julai 2018 hadi Juni 2019. Masuala yaliojadiliwa ni pamoja na elimu, afya, kilimo, mifugo, umeme, maji, miundombinu ya barabara, usalama wa raia na uhifadhi wa wanyama pori.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. Box 23 Liwale
Simu ya Mezani: +255 (0) 737 187 605
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2018 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.