Mkurugenzi Mtendaji (W) Bi Luiza O. Mlelwa afurahishwa na maendeleo ya mradi wa kitalu nyumba kwa vijana wa Halmashauri ya Liwale. Aliyasema hayo jana Julai 5 alipofanya ziara katika mradi wa kitalu nyumba uliopo katika kijiji cha Mungurumo katika eneo la ofisi za Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika. Mradi huu umetoa fursa kwa vijana 80 (Me 30 na Ke 50) kutoka katika kata za Liwale mjini, Nangando, Likongowele, Mangirikiti, Kichonda, Mbaya, Liwale B, na Makata waliohamasika kuja kushiriki na kujifunza Kilimo cha Umwagiliaji wa matone kwa kutumia kitalu nyumba. Mpango huu wa mafunzo ya Kilimo cha matone kwa kutumia Kitalu nyumba unalenga kuwezesha vijana kuwa na mbinu na maarifa ya Kilimo cha kisasa chenye kuzingatia teknolojia, pia kukukabiliana na utekelezaji wa agenda ya viwanda kwa kuongeeza thamani ya mazao yatokanayo na bustani. Aidha mpango huu pia unalenga kuchochea vijana kujiajiri kupitia shughuli za kilimo. Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji (W) amewataka Mratibu wa Mradi Ndg. David Mgalula na Afisa Maendeleo ya Jamii (W) Ndg. Mkoveke kuendelea na kasi hiyo ya utekelezaji pia aliwashauri wapande mazao ya bustani kama mipapai, migomba na mbogamboga.
Along Nachingwea Road opposite DDD Quarters
Sanduku la Posta: P.O. Box 23 Liwale
Simu ya Mezani: +255 (0) 737 187 605
Mawasiliano ya mkononi:
Baruapepe: ded@liwaledc.go.tz
Hakimiliki 2018 © Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Haki zote zimehifadhiwa.